Karibu katika njia ya Imani katika Bwana katika Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume

Kanuni ya Imani

Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi,/ mwumba mbingu na dunia./ Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu;/ aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu,/ akazaliwa na Bikira Maria,/ akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato,/ akasulubiwa, akafa, akazikwa,/ akashukia kuzimu;/ siku ya tatu akafufuka katika wafu;/ akapaa mbinguni;/ amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi;/ toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,/ Kanisa takatifu katoliki,/ ushirika wa Watakatifu,/ maondoleo ya dhambi,/ ufufuko wa miili,/ uzima wa milele. Amina.

Jinsi ya kukiri imani na kuamini

 • Kukiri kanuni ya imani
 • Kubatizwa

Kufuata Imani

 • Kushika Amri za Mungu na za Kanisa
 • Sala na Ibada
 • Kuyafahamu mafundisho ya imani na misingi ya imani
 • Kusoma Katekisimu ya kanisa kama msingi wa Imani
 • Kupokea sakramenti Takatifu ubatizo,kitubio,ekaristi,kipaimara n.k

  Matumaini ya imani yetu

  ufufuko wa miili,/ uzima wa milele.

  Tembelea Kanisa Katoliki lililoko Jirani na wewe kwa msaada na maelezo zaidi