Miujiza‎ > ‎Mwandishi‎ > ‎Maandishi‎ > ‎Sala‎ > ‎

SALA YA TOBA

SALA YA TOBA

Ee Mungu wangu unihurumie kwa wingi wa fadhili zako na rehema zako unitakase dhambi zangu kwa maana nimekua mpumbavu. Nimekukosea wewe pekee. Uovu wangu unaujua waziwazi. Hakuna hata neno moja linalofichika kwako. Unihurumie unirehemu mimi niliyeanguka mpaka ardhini. Uovu wangu unanielemea. Nimefika mahali pasipofaa nimechoka kwa kupiga kite kwangu. Ee Mungu Unirehemu unisikilize unisaidie. Ee Mungu, Mungu wa wokovu wangu. Amina.

Tar 11/1/2014, By Shine, Melkisedeck L.

Comments