Sala zetu‎ > ‎

Kumbuka kwa Mt. Yosefu

posted Nov 2, 2014, 11:00 AM by Melkisedeck Leon
Kumbuka

Kumbuka ee mchumba safi wa Bikira Maria, haijasikika hata mara moja umemwacha mtu aliyeomba msaada wako, nami kwa matumaini hayo nakukimbilia wewe na kuomba ulinzi wako, ee baba mlishi wa mkombozi, usikatae ombi langu nyenyekevu, bali kwa wema wako unisikilize na unijibu. Amina
Comments