Sala zetu‎ > ‎

SALA KWA MT.AGATHA,BIKIRA,SHAHIDI NA MSIMAMIZI WA WAUGUZI

posted Nov 2, 2014, 9:57 AM by Melkisedeck Leon   [ updated Nov 2, 2014, 10:50 AM ]

SALA KWA MT.AGATHA,BIKIRA,SHAHIDI NA MSIMAMIZI WA WAUGUZI

Ee Mungu baba wa mbinguni,tunakushukuru kwa kutupatia Watakatifu wako ambao wapo pamoja nawe Mbinguni wakituombea, miongoni mwao ni Mt.Agatha.Tunakuomba kwa maombezi yake na kwa huruma yako utuijalie afya njema ya roho na mwili.
Ee baba Mungu Kanisa lako limemweka Mt.Agatha kuwa msimamizi wa wauguzi wote,tunakuomba kwa maombezi yake utujalie sisi wauguzi wote tujitoe kwa moyo wote katika kuwahudumia Wagonjwa kwa upendona kuwafariji.
Mpendwa Mt.Agatha ambaye kwa ujariri mkubwa ulivishinda vishawishi kwa kupitia mateso makali.Tunakuomba uteombee kwa Mungu atujalie sis wanajumuiya ambao tumekuchagua wewe kuwa msimamizi wa Jumuiya yetu tuweze kuvishinda vishawishi vinavyotukabili na tuweze kujitoa kikamilifu katika kuijenga na kuiendeleza jumuiya yetu.
Pia tunawaombea Waonjwa wote Mungu awaponye kuwafariji katika mahangaiko yao yote.
Baba yetu……….Salamu maria……………Atukuzwe Baba……..
Mt.Agatha somo na mlinzi wa Jumuiya yetu…UTUOMBEE….X3.
Comments