Sala zetu‎ > ‎

SALA YA KUOMBA MAOMBEZI MT.FRANSISCO WA ASISI

posted Nov 2, 2014, 10:09 AM by Melkisedeck Leon   [ updated Nov 2, 2014, 10:10 AM ]

SALA YA KUOMBA MAOMBEZI  MT.FRANSISCO WA ASISI

Ee Bwana unifanye niwe chombo cha amani yako,
Palipo na chuki nilete mapendo
Palipo na makosa nilete msamaha
Palipo na shaka nilete imani
Pasipo na matumaini nilete tumaini
Palipo na giza nilete mwanga
Palipo na huzuni nilete furaha.
Ee Bwana unisaidie nitamaini sana:
Kufariji kuliko kufarijiwa
Kufahamu kuliko kufahamiwa
Kupenda kuliko kupendwa
Kwa kuwa:
Ni katika kutoa ndipo tunapokea
Ni katika kusamehe ndipo tunaposamehewa
Ni katika  kifo ndipo tuna zaliwa katika uzima wa milele.
                          AMINA   

Comments