Sala zetu‎ > ‎

SALA YA KUOMBEA FAMILIA.

posted Nov 2, 2014, 7:09 AM by Melkisedeck Leon
SALA YA KUOMBEA FAMILIA.
Ewe Mungu Mwenyezi, sisi kama familia tunakushukuru kwa zawadi ya Mama Kanisa Katoliki ambaye siku zote hutupatia malezi bora kwa ajili ya wokovu wetu. Kanisa halichoki kutuhimi za tutafakari na kuishi utakatifu wa familia ya Nazareti ya Yesu, Maria na Yosefu. Familia hii iliishi upendo uliojengwa kwa fadhila za imani, uaminifu, utii, uvumilivu na upole hata wakawa watakatifu.
Tunapoadhimisha mwaka wa Familia, tunaiweka mbele yetu
familia ya Nazareti iwe dira, baraka
na mfano kwa familia zetu.
Tunakushukuru Baba kwa ajili ya familia zote zinazojitahidi kuishi fadhila hizo za Familia takatifu na tunakuomba uzidi kuwaimarisha wanandoa ili tupate kwao mifano mingi na bora ya kuigwa.
Ee Bwana, tunaomba Roho Mtakatifu atuangazie tuweze: kutambua familia kuwa Kanisa la nyumbani na shule ya imani na upendo; kuimarisha familia kwa sala, sakramenti na tunu za kiinjili na kushirikiana kwa heshima katika familia kwa usitawi wa roho na wa mw ili kwa wanafamilia
wote. Tunaziombea familia zetu na Jumuiya Ndogondogo za Kikristo ziwe bustani bora
na salama
za kuchipusha na kulea miito mitakatifu ya Ndoa, Utawa na
Upadre.
Tunawaombea v
ijana na watoto
wetu
Uchaji wa Mungu ili
w
awe
na bidii ya kuji
tunza kwa kushika amri za Mungu
na
kuishi
fadhila za kiinjili, wawe na roho ya kimisionari yaani
walipende
Kanisa na
kuwa na moyo
wa kueneza
ufalme wako kwa matendo ya imani
.
Baba wa huruma, tunakukabidhi familia zenye
misukosuko ya mafarakano
, ulevi, ubin
afsi,
uregevu
-
dini, uvivu,
ushirikina,
hofu,
magonjwa sugu na mengineyo yenye kuleta huzuni; kwa hisani yako uwape neema, mwanga na
nguvu za
kuanza maisha mapya yenye
amani, waweze
kufurahia
upatanisho na
uponyi wa pendo lako la kibaba
kati yao
.
Tunaomba
toba na msamaha kwa ukatili, manyanyaso na
hata
mauaji katika familia
zetu
na uwaponye wote
waliojeruhiwa kwa maneno, matendo na makwazo
ya aina yeyote.
Aidha tunakuomba uwe kitulizo na faraja kwa wagonjwa na wazee, pia
tegemeo la yatima na wajane.
Wen
ye
matatizo ya kiafya au ya kijamii wasikate tamaa bali waunganishe hali zao na msalaba wa Mwanao na kukutumaini
wewe Mweza yote.
Jamii iwajibike n
ao
kwa ku
zi
jali haki zao
na kuwapa misaada wanayohitaji.
Tunakuomba ubariki miradi na kazi zetu ili familia
zipate usitawi na maendeleo
; na utujalie hekima ya
kukushukuru kwa maisha ya haki
, amani
na ukarimu
na
mwisho tu
ka
imbe sifa zako
pamoja na familia Takatifu
ya Yesu
,
Maria na Yosefu
na jeshi lote la mbinguni
.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wet
u.
Amina.
Baba yetu...
.....
Salamu Maria
....
...Atukuzwe Baba...
....
Comments