Sala zetu‎ > ‎

Sala zilizo muhimu na za kila siku

posted Oct 31, 2014, 5:12 AM by Melkisedeck Leon   [ updated Nov 2, 2014, 9:10 AM ]
SALA YA IMANI
MUNGU WANGU, NASADIKI MANENO YOTE LINALOSADIKI , NA LINALOFUNDISHA KANISA KATOLOKI  LA ROMA:KWANI NDIWE ULIYEFUNDISHA HAYO,WALA HUDANGANYIKI, WALA HUDANGANYI.AMINA

SALA YA MATUMAINI
MUNGU WANGU, NATUMAINI KWAKO NITAPEWA KWA NJIA YA YESU KRISTU,NEEMA ZAKO DUNIANI NA UTUKUFU MBINGUNI, KWANI NDIWE ULIYEAGANA HAYO NASI, NAWE MWAMINI.AMINA

SALA YA MAPENDO
MUNGU WANGU, NAKUPENDA ZAIDI YA CHO CHOTE, KWANI NDIWE MWEMA MWEMA, NDIWE MWENYE KUPENDEZA. NAMPENDA NA JIRANI YANGU KAMA NAFSI YANGU, KWA AJILI YAKO.AMINA.

SALA YA KUTUBU
MUNGU WANGU, NIMETUBU SANA DHAMBI ZANGU, KWANI NDIWE MWEMA NDIWE MWENYE KUPENDEZA, WACHUKIZWA NA DHAMBI. BASI SITAKI KUKOSA TENA, NITAFANYA KITUBIO, NAOMBA NEEMA ZAKO NIPATA KURUDI AMINA.

SALA KWA MALAIKA MLINZI
MALAIKA MLINZI WANGU, UNILINDE KATIKA HATARI ZOTE ZA ROHO NA ZA MWILI AMINA
Comments