Mathayo 5:1-12

posted Oct 31, 2014, 3:02 AM by Melkisedeck Leon   [ updated Oct 31, 2014, 4:57 AM ]

1  Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia;

2  akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema,

3  Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

4  Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.

5  Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.

6  Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.

7  Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.

8  Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.

9  Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.

10  Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

11  Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.

12  Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

Comments